Sunday, January 9, 2011

Mapenzi ni nini Maishani?


Mapenzi ni idadi kadhaa ya hisia zinazohusiana na mahaba [1] pendo na hata upendo wa Kimungu.

Neno "kupenda" linaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ("Napenda chakula hicho"), hadi mvuto mkali kati ya watu ( "Nampenda mume wangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi wa dhana hii, hata ikilinganishwa na hali zingine za kihisia.







Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya finyu pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba na ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usiohusisha ngono [2] hadi umoja wa kina au ibada ya upendo] wa kidini. [3]

Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano kati ya binadamu na, kutokana na umuhimu wake mkuu wa kisaikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika sanaa



Ufafanuz





Neno la Kiingereza "love" linaweza kuwa na maana tofauti, lakini zinazohusiana, katika miktadha tofauti. Mara nyingi, lugha nyingine hutumia maneno mbalimbali kueleza baadhi ya dhana tofauti ambazo lugha ya Kiingereza hutumia neno "love" kurejelea; mfano mmoja ni wingi wa maneno ya Kigiriki yanayorejelea "mapendo". Tofauti za utamaduni katika kufafanua mapenzi hivyo, hufanya liwe jambo gumu kuanzisha ufafanuzi bia wowote. [4]

Ingawa desturi au chanzo cha mapenzi ni suala ambalo hujadiliwa mara kwa mara, sura tofauti ya neno hili zinaweza kuwekwa wazi kwa kuamua ni nini ambacho sio mapenzi. Kama njia ya kawaida ya kuonyesha hisia chanya (aina kubwa ya kupenda), mapenzi kwa kawaida hulinganuliwa na chuki (au kutojali); kama upendo ambao umegemea zaidi kwenye uhusiano wa kirafiki kuliko wa kingono, mapenzi kwa kawaida hulinganuliwa na tamaa, na kama uhusiano kati ya watu, unaohusisha mahaba, mapenzi hulinganuliwa na urafiki, ingawa fdesturi zingine za neno mapenzi zinaweza kutumika kwa urafiki wa karibu katika miktadha fulani.

Wakati yanapojadiliwa katika hali dhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea upendo kati ya watu, hisia alizo nazo mtu kuhusu mtu mwingine. Mapenzi mara nyingi yanahusisha kutunza au kujiainisha na mtu au kitu, ikiwa ni pamoja na nafsi ya mtu.

Aidha, katika tofauti za-kiutamaduni katika kuelewa mapenzi, mawazo kuhusu mapenzi pia yamebadilika sana na mpito wa wakati. Baadhi ya wanahistoria wanahusisha dhana za kisasa za mapenzi ya kimahaba na Ulaya wakati au baada ya enzi ya kati, ingawa kuwepo kwa mahusiano ya kimahaba kabla ya wakati huo kunaonyeshwa na ushairi wa kimapenzi wa kale. [5]


Mikono miwili ikiunganika kutengenezea umbo la moyo.Kutokana na utata na udhahania wa mapenzi, mjadala juu ya mapenzi kwa kawaida hupunguzwa hadi maneno yaliyopitwa na wakati, na kuna mithali kadhaa kuhusu mapenzi, mojawapo ikiwa ile ya Vergilio ya kuwa "Pendo hushinda yote" na ile ya Beatles "All you need is love" (Unachohitaji ni mapenzi tu).

Bertrand Russell anaelezea mapenzi kama hali ya "thamani kamili", kinyume na thamani inayobadilika.

Mwanafalsafa Gottfried Leibniz alisema kwamba mapenzi ni "kuwa na furaha tele kutokana na furaha ya mwingine."



Mapenzi yasiyohusishwa na mtu maalum




Mtu anaweza kusemekana kuwa anapenda nchi, kanuni, au lengo ikiwa anaithamini sana na kuizingatia kwa makini. Vilevile, mapenzi ya huduma za huruma na wafanyakazi wa kujitolea ' "upendo" ya kazi yao yanaweza kutokana na mapenzi yasiyohusishwa na kitu pamoja na utu na imani za kisiasa badada ya mapenzi kati ya watu. Watu pia wanaweza "kupenda" vitu, wanyama, au shughuli ikiwa wao wenyewe watajitolea kutagusana au kwa vinginevyo kujihusisha na vitu vile. Ikiwa tamaa ya kingono pia inashirikishwa, hali hii inaitwa 'paraphilia'.

No comments:

Post a Comment