Sunday, October 3, 2010

Uchungu wa Mwana..



Mama mmoja nchini Israel amenusurika kufariki baada ya kujirusha toka ghorofa ya nne baada ya kuona watoto wake wawili wamejirusha chini kupitia dirishani.
Mama mmoja mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa mji wa Tel Aviv nchini Israel, amenusurika kufariki baada ya kujirusha toka kwenye ghorofa ya nne.

Mama huyo alichukua uamuzi huo wa haraka baada ya kuona watoto wake wawili wamejirusha chini kupitia dirishani toka kwenye nyumba yao iliyopo ghorofa ya nne.

Mama huyo aliamua kutumia dirisha hilo hilo kujiua mwenyewe kwa kujirusha hadi chini.

Bahati nzuri kwao, mama na watoto wake wote wawili walinusurika maisha yao ingawa wamevunjika vunjika viungo vingi vya miili yao.

Mtoto mmoja alikuwa wa kike mwenye umri wa miaka 7 wakati mtoto wake wa pili alikuwa wa kiume mwenye umri wa miaka 5.

Hali ya mtoto wa kike inaendelea vizuri lakini hali ya mtoto wa kiume si ya kuridhisha.

Baada ya kufikishwa hospitali mama wa watoto hao alipoulizwa sababu ya kujirusha toka ghorofa ya nne alisema kuwa alifikiria watoto wake ndio wameishafariki hivyo na yeye aliamua kujiua.

No comments:

Post a Comment